Nawashukuru sana wadau wa blogu ya mtandao vijana kwa ushirikiano na heshima ambayo mnanipa ya kurusha hizi habari kila siku. jamani mila na desturi haziwezi kufa wala kwisha maana ndizo zinazotambulisha jamii ya watu popote pale duniani.
>
picha hii inaonyesha muheshimiwa mkubwa sana duniani au Raisi wa taifa lenye nguvu kwa namna zote akipokea salamu kutoka kwa mtoto. Ameinama kama heshima ya kupokea salamu hii ambayo nafikiri inapatikana Afrika Mashariki tu ambako pia ndiko asili ya bwana barack Obama. salamu hii imezoeleka kutoka kwa mdogo kwenda kwa mkubwa ikisema Shikamoo na kuitikia "marahaba".
No comments:
Post a Comment