KARIBUNI SA

Thursday, July 28, 2011

Lisu, Lema na Mchungaji Msigwa watolewa bungeni leo

Naibu Spika Job Ndugai akiwaamuru wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu, Mchungaji Peter Msigwa na Godbless Lema kutoka ndani ya bunge leo mara baada ya wabunge hao kudaiwa kuvunja kanuni ya bunge ya kuongea bila ruhusa ya Naibu spika.

Askari polisi wa bunge wakiwasindikiza Tundu Lisu(Kulia)Mchungaji Peter Msigwa (Kushoto) na Godbless Lema (katikati) watoke njee ya viwanja vya bunge mara baada ya Naibu spika Job Ndugai(hayupo Pichani) kutoa amri hiyo wakati wa bunge asubuhi ya leo

Wa pili kulia ni Muheshimiwa John Mnyika mbunge wa Ubungo akiwasindikiza wabunge wenzake kutoka ndani ya bunge hilo leo asubuhi Dodoma

Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA)Godbless Lema akiingia ndani ya gari na huku mbunge wa Singida mashariki (CHADEMA)Muheshiwa Tundu Lisu akisubiri kuingia kwenye gari mara baada Naibu spika Job Ndugai kuwaamuru watoke bungeni kwa kuvunja kanuni ya bunge ya kuongea bila ruhusa.