KARIBUNI SA

Saturday, May 15, 2010

UCHAGUZI UINGEREZA MPAKA KUUNDA SERIKALI

Uchaguzi umekuwa una matukio mengi hasa baada ya kura kutokutosha kwa waziri mkuu aliyepita muheshimiwa Gordon Brown

Gordon Brown wa Chama cha Labour Party na David Cameroon wa Chama cha Conservative na watatu ni Nick Glegg wa chama cha Liberal Democrats.

Waziri Mkuu nchini Uingereza Mh. Gordon Brown atajiuluzu kuwa kiongozi wa Chama Cha Labour Party.

Mh. Brown's ametangaza uamuzi huo baada ya Chama chake kushindwa kupata kura za kuongoza nchi katika uchaguzi
David Miliband amepewa nafasi kubwa ya kuweza kushika nafasi ya kuingoza Labour Party endapo Gordon Brown ataachia ngazi.

Bw. Miliband ambaye kwa hivi sasa ni Waziri wa Mambo ya Nje yupo mstari wa mbele katika king'ang'aniro cha kugombea kukiongoza chama Labour Party.

Sehemu nyingi za kuchezea pata potea (Kamali) kama Paddy Power, William Hill na Ladbrokes zimetokea kumeweka katika nafasi ya juu ya kuweza kushinda.

William Hill wamesema watu zaidi ya 25 na kiasi kisichopungua paundi £1000 zimewekezwa kwaajili ya nani atakuwa kiongozi wa Labour Party.




Gordon akimuaga malkia na ameondoka Downing Street, Buckingham Palace akiwa ameshikana mikono na na mkewe Saraha na watoto wao John na Fraser.


Vyama viwili vya siasa nchini Uingereza Liberal Democrats na Conservative Party vinakutana jijini London kujadili jinsi gani watavyoweza kuunda serikali ya pamoja ya kuingoza nchi.

David Cameron wa chama cha Conservatives, chama ambacho kimepata kura nyingi kushinda vyama vyote katika uchaguzi uliofanyika Alhamisi lakini kimeshindwa kufikia idadi ya viti 326 vya kuweza kuingoza nchi, hivyo basi wanahitaji ushirikiano na chama cha Liberal Democrats kinachoongozwa na Nick Glegg kuweza kuunda serikali.


Serikali mpya ya Uingereza inayoongozwa na Mh. David Cameron imejipunguzia mishahara kwa asilimia 5% kwaajili ya kupunguza bajeti ya rekodi ya madeni.

Vyama vya Conservatives na Liberal Democrats Vimekubaliana siku ya Jumanne kuweza kushirikiana katika kupunguza madeni yanayoikabili nchi na pia kupambana na hali ngumu ya uchumi wa nchi.

Baraza zima la Mawaziri limekutana kwa mara ya kwanza kujadiliana mikakati ya kuendesha nchi na kujipunguzia mishahara.

Waziri Mkuu David Cameron mshahara wake utapungua toka Paundi £150,000 mpaka kufikia Paundi £142,000 na viongozi wa chini yake watapokea Paundi zisizozidi £135,000 kwa mwaka.

Mawaziri wote watapunguziwa mishahara yao kwa muda wa miaka 5. Kitendo hicho kitasaidia kuokoa kiasi cha Paundi millioni tatu za Kiingereza.

No comments:

Post a Comment