Vyuo vikuu kuna nafasi nzuri za uongozi ambazo zinaweza kumuandaa kila anayependa kuwa kiongozi au kulitumikia taifa kujifunza na kupata uzoefu. ila kwa mda mrefu nimekuwa nikitafakari je ni kweli kwamba hawa wanaoomba dhamana kwa wananchi au wanachuo wenzao kuwawakilisha ni kweli wanakuwa na nia hiyohiyo tu au kuna maslahi ambayo wanatarajia kupata. Mwaka Jana chuo kikuu cha Dodoma kilichagua raisi wake ambaye alikuwa akitokea katika chuo cha sayansi ya mawasiliano ambaye alifahamika kama Raymond Magambo. Baada tu ya kuchaguliwa akapata safari ya kwenda China, hizi ni baadhi ya picha ambazo Raisi ambaye anamaliza mda wake alipata kupiga akiwa china. Yaaani ilikuwa ni bonge la starehe ya kufa mtuuuuu..
muheshimiwa Magambo akianza safari yake ndani uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere, Dar
muheshimiwa akiwa ndani ya pipa lijulikanalo kama Quatar airways akielekea Doha, Quatar.
hapa mkuu akitazama show huko Beijing, China
hapa Raisi Magambo akiwa na warembo katikati ya mji wa Beijing ambapo ni mji wenye msongamano mkubwa wa watu
ni moja ya hotel kubwa beijing china
huu ni mda wa menu
sasa nafikiri unaweza kupata jibu au swali kwa nini wengi wanagombea uongozi vyuoni wanakuwa na dhamira ipi? hasa na baada ya kusikia kwamba kuna safari za kwenda china na kadhalika
No comments:
Post a Comment