KARIBUNI SA

Tuesday, March 16, 2010

VIONGOZI WA LOYOLA ALUMNI ASSOCIATION( LAA) WATEMBELEA UDOM


Mwisho wa wiki tarehe 13 mwezi wa 3 mwaka huu 2010, viongozi kutoka makao makuu ya asasi ya wanafunzi waliosoma katika shule ya Loyola walitembelea chuo kikuu cha dodoma na kujiona mazingira mazuri ya chuo ambacho kinaendelea kujengwa. viongozi hao ambao ni janeth ambaye ni katibu, joseph ambaye ni muheka hazina, felix na sia lyimo wote ambao ulikuwa ni msafara wa watu wanne. siku hiyo viongozi hao walipata mda wa kuongea na wanafunzi ambao walimaliza shule ya loyola na sasa wanachukua shahada yao katika chuo hicho. walisisitiza sana juu ya kuwa na upendo na kauli mbiu yao inayosema "men and women for others". baada ya kutoa nasaha zao wanafunzi hao walipata mda wa kuimba wimbo wao wa taifa wakiwepo chuon hapo. viongozi hao waliwashukuru sana viongozi wa asasi katika chuo kikuu cha dodoma kwa mapokezi mazuri.

No comments:

Post a Comment