![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgA6g6kEZVSB_rlwby2_b89fN2nuakrxCzjoEPORWxpYWvodHAbkOY71CRCx54ZSqPF91LWKYMzAGsTIBPMhqRWdFH-zihuzWs64NdQDe2TOmDC0Gpt-mTK8h2hRVRKcvTMOShSI0ws6XXj/s400/udom.jpg)
Hapa chuoni michakato ya kuunda kambi inaendelea ambayo inaonyesha kila mmoja yupo kimaslahi zaidi ya kupata uongozi na kuendeleza usela au ushikaji. Mwaka jana yalitokea kama haya ambapo muheshimiwa Teri Gilead ambaye alikuwa mpinzani mkubwa wa Ambrose alikuwa na haya ya kusema pale alipohojiwa na Kubwakuliko alikuwa na haya ya kusema
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhliNjyLTrguO7kRBS4Glh_ZrIkmTqDZqWm57sHHmNWHuG1QdtcArIi0YkupTHnLk3AGvKFpVyamREhfO2ARJTsKil7CVQ8AvwScJKYRGxEeL44s5iFOy8IErtCHVnqiOYjOqkf6Brm3PP_/s400/teri.jpg)
Mgombea Urais aliyepita ssh
Muheshimiwa Gilead Terry
TERRY: Kwanza napenda kukushukuru sana kwa kufika hapa, umekuwa kama tone la mvua jangwani. Serkali hii bana ni serikali ya kishkaji mnoooo
MWANDISHI: Una maanisha nini mkuu?
TERRY: Yaani, uwezi kuamini waziri mkuu wenu ni mwanachumba mwenzake “roommate” athari ya hili ndo kama unavyo ona sasa anakuwa anamjali yeye zaidi kulliko watu wengine
MWANDISHI: Alikuwa roommate wake kabla au baada ya kuwa Rais?
TERRY: Kabla ya kuwa rais, kifupi ni kwamba serikali haikujiaanda kabisa kuongoza ,wanavyo tufanyia ni, “foolishness of the highest level”
Sasa ni vyema kufanya maamuzi ambayo yatatuletea maslahi makubwa kwetu kwa kipindi kijacho na sio maslahi binafsi. Maana kuna msemo usemao “ SI KILA AKUTAZAMAYE ANAKUONA” kwa hiyo tusiwatupia mpira wengine kwamba wao ndo wahusika lakini wote tunapaswa kushiriki pamoja katika hili
Kutoka kwa mdau
Manase Kavishe
No comments:
Post a Comment