Wednesday, April 21, 2010
SIMBA MABINGWA WA LIGI KUU YA VODACOM 2010/2011
wachezaji wa timu ya Simba wakiwa na kombe lao la ubingwa walilokabidhiwa mara baada ya kumalizika kwa mechi kati yao na watani zao Yanga katika mtanange wa kukata na shoka uliomalizika katika uwanja wa Taifa.Simba ndio mabingwa wapya wa ligi kuu ya Vodacom 2010/11
mashabiki wa simba wakishangilia kwa bidii ndani ya uwanja wa taifa
Mshambuliaji wa Yanga Jerson Tegete akishangila mara baada ya kufunga bao dhidi ya Simba muda mfupi baada ya kuchukua nafasi ya Bonifac Ambani.Katika mchezo huo Simba ilishinda mabao 4-3 huku mawili yakifungwa na Mussa Hassan Mgosi.
mashabiki wa Yanga wakishangilia timu yao ndani ya uwanja wa taifa dsm
simba ndo wanajiamini sana na kubaki kuwashangaa Yanga au ndo utani wa Jadi....
UCHAGUZI UDOSO WAZINDULIWA RASMI JUMATANO YA TAREHE 15.04.2010
siku ya jumatano iliyopita chuo kikuu cha Dodoma,uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ulizinduliwa rasmi na mlezi wa wanafunzi au dean of student katika ukumbi mkubwa chimwaga ukifuatiwa na mdahalo wa viongozi ambao wanagombea nafasi mbalimbali ikiwemo mwenyekiti wa chuo kizima na makamu wenyeviti wa kila kitivo, mlezi huyo wa wanafunzi alisisitiza kuwa tunabidi tufanye siasa kwa amani na tusichafue majina ya watu kama mwaka jana ilivyokuwa katika uchaguzi wa pili wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu hiki ambacho kinategewa kuwa chuo kikubwa afrika mashariki na kati. Mlezi huyo aliendelea kusisitiza kwamba wote tunapaswa kushiriki kwenye uchaguzi huu kwa njia ya amani na tuchague viongozi tunaowahitaji. Alitoa mfano wa chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda ambapo mwanzo mwa mwaka huu wanafunzi walipoteza maisha kutokana na shughuli za kisiasa ambazo zilikuwa zikiendelea hapa. Pia mlezi huyo aliendelea kusema kwamba wao kama utawala watakuwa bega kwa bega kusimamia uchaguzi huo ufanyike kwa njia ya amani
Hapa chuoni michakato ya kuunda kambi inaendelea ambayo inaonyesha kila mmoja yupo kimaslahi zaidi ya kupata uongozi na kuendeleza usela au ushikaji. Mwaka jana yalitokea kama haya ambapo muheshimiwa Teri Gilead ambaye alikuwa mpinzani mkubwa wa Ambrose alikuwa na haya ya kusema pale alipohojiwa na Kubwakuliko alikuwa na haya ya kusema
Mgombea Urais aliyepita ssh
Muheshimiwa Gilead Terry
TERRY: Kwanza napenda kukushukuru sana kwa kufika hapa, umekuwa kama tone la mvua jangwani. Serkali hii bana ni serikali ya kishkaji mnoooo
MWANDISHI: Una maanisha nini mkuu?
TERRY: Yaani, uwezi kuamini waziri mkuu wenu ni mwanachumba mwenzake “roommate” athari ya hili ndo kama unavyo ona sasa anakuwa anamjali yeye zaidi kulliko watu wengine
MWANDISHI: Alikuwa roommate wake kabla au baada ya kuwa Rais?
TERRY: Kabla ya kuwa rais, kifupi ni kwamba serikali haikujiaanda kabisa kuongoza ,wanavyo tufanyia ni, “foolishness of the highest level”
Sasa ni vyema kufanya maamuzi ambayo yatatuletea maslahi makubwa kwetu kwa kipindi kijacho na sio maslahi binafsi. Maana kuna msemo usemao “ SI KILA AKUTAZAMAYE ANAKUONA” kwa hiyo tusiwatupia mpira wengine kwamba wao ndo wahusika lakini wote tunapaswa kushiriki pamoja katika hili
Kutoka kwa mdau
Manase Kavishe

MDAU WA GLOBU AONANA NA VIONGOZI WA NCHI BUNGENI
Wednesday, April 14, 2010
ENZI ZA UONGOZI WA MWALIMU
Friday, April 9, 2010
POLISI WAWAPIGA RAIA RISASI
Polisi wilayani Rorya mkoa wa Mara, wamefyatua risasi za moto katikati ya raia na kuua watu wawili na kuwajeruhi wengine tisa.
Idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwani wakati tunakwenda mitamboni habari zilionyesha kwamba baadhi ya majeruhi walikuwa na hali mbaya.
Waliokufa katika tukio hilo, wamejulikana kuwa ni Iranda Matoka (26) na Abbas Adek (23).
Aidha, majeruhi walitajwa kwa majina ya Wandiba Nyamkondya (26), Julius Nduku (26), Aziz Mganga (18), Sanga Matiko (32), Isiro Magesa (38), Ezekiel Robert (15), Ramadhani Magige (32), Musoba Rhobhi (32) na Leonard Kahanga.
Tukio hilo lilitokea jana, wakati askari hao walipokabiliana na wakazi wa kijiji cha Moharango, walioandamana kwenda kituo cha polisi Utegi, wakitaka kuachiwa huru kwa wazee wanne wa mila.
Wazee hao waliojulikana kwa majina ya Kahanga Mwando, Odila Runyola, Saba Kahanga na Wasaga Mganga, walikamatwa kwa madai ya kutishia kumroga na kumuua mkazi wa kijiji hicho, Joseph Ngondi.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa Nipashe, madai ya kumroga na kumuua Ngondi, yalitokana na hatua ya mwanakijiji huyo kufyeka mlima Nyabigiga, unaosadikiwa kutumika kwa masuala ya tambiko.
Watu walioshuhudia tukio hilo, waliliambia Nipashe kuwa baada ya wazee hao kukamatwa na kuwekwa ndani juzi, wanakijiji hao waliandama kwenda kituoni hapo kwa lengo linalodhaniwa kushinikiza kuachiwa kwa wazee wa kijiji, ndipo walipokabiliana na polisi waliokuwa na silaha zenye risasi za moto.
``Tulisikia milio ya risasi na baadaye vilio huku watu wakikimbia hovyo,`` mmoja wa mashuhuda ambaye jina lake halikupatikana, alisema.
Miili ya watu waliokufa na majeruhi ilipelekwa katika hospitali ya wilaya ya Tarime.
Majeruhi katika tukio hilo, miongoni mwao wakiwa katika hali mbaya, walijeruhiwa mikononi, miguuni, mgongoni na mapajani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Liberatus Barlow, hakupatikana jana kuzungumzia tukio hilo.
SOURCE: Nipashe

WASHINDI WA NITASOMA SCHOLARSHIP PROMOTION WAPATIKANA
Bi.Venancia Donald akipokea zawadi ya NITASOMA MOBILE 1 kwa niaba ya Witness Lucas wa Tumaini University Iringa. Akikabidhi zawadi hizo kulia ni Levis Paul Campaign & Marketing Manager 4layers (T) Ltd. Shughuli hio fupi ilifanyika leo katika ofisi ya kampuni hio iliyoko Msasani Dar es salaam
Bw. Valentino J. Mhoja kutoka Dar es salaam Institute of Technology akipokea zawadi ya NITASOMA MOBILE 3 kutoka 4Layers (T) Ltd's Levis Paul akikabidhi zawadi hio Kushoto ni Bi. Venancia Donald.
Akielezea zaidi Bwana Levis Paul alisema promosheni hio ya NITASOMA inakuja juu kwa kasi ikiwa hii ni wiki ya tatu tangu kuanza rasmi 15.03.2010 na kwamba ni matarajio yao kuchagua washindi watatu kwa vitabu vya sekondari, mwanafunzi mmoja simu ya mkononi na laptop katika wiki ya nne yaani jumatatu ijayo.
Alitoa changamoto kwa walengwa walio vyuoni na mashuleni kushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi NITASOMA UNI, au NITASOMA HIGH au NITASOMA SEC kwenda 15767 ili kushiriki katika promotion hii.
ELIMU KWANZA.
info.nitasoma.com
www.nitasoma.blogspot.com
Wednesday, April 7, 2010
RAIS JAKAYA KATIKA SHEREHE ZA KUMUENZI MZEE KARUME
Jana tarehe 6 mwezi 4 mwaka 2010 muheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ahutubia vijana wa UVCCM Zanzibar katika kumuenzi karume.Rais pia alipoke maandamano kutoka kwa vijana hao.
Monday, April 5, 2010
MAMBO YA PASAKA NDANI YA BOBBYS LODGE DOM
Jumapili ya pasaka wanafunzi wa chuo kikuu cha dodoma ambao walipata kusoma shule ya sekondari loyola mabibo, dar. vijana hawa loyola alumni association(LAA) wakiambatana na marafiki wenzao walisherekea pasaka kwa namna ya tofauti pale walipoandaa get together party au sherehe ya pamoja na marafiki. sherehe hii ilifanyika katika lodge moja mjini dodoma inayofahamika kama Bobbys ambayo inamilikiwa na mbunge wa dodoma mjini muheshimiwa Madeje
mdau nikiwa na wadau wenzangu
muheshimiwa Ephaim Madeje akiwa na mke wake
hapa Gervas anacheza pakacha pakacha...
hapa dj John kutoka chuo cha sayansi na mawasiliano au info akishughulikia swala la muziki vilivyo.
kushoto ni brian, salum, teri , kanal, manase au mdau mtandao vijana naye alikuwepo
dah usipime watu waliinjoy walikula misosi ya maana. yaani ni kuku na chipsi kama picha inavyoonekana hapo juu.
kushoto ni EVELYNE, JOYCE na AMMY SANGA
kushoto ni mwenyekiti wa shughuli mr. PAUL MASHINGIA, MAKENE MGENI, DAVID

Saturday, April 3, 2010
PASAKA NJEMA WADAU
Mimi kama mdau wa globu ya mtandao wa vijana ninawatakia wapendwa wote sikuku njema ya pasaka. pasaka ni sikuku ambayo inaadhimishwa na wakristo duniani kote ambako tunaamini kwamba Yesu kristo alikufa msalabani na siku ya tatu akafufuka. hii yote ni upendo wa Mungu Baba kwa ajili ya wanadamu. Sasa sikukuu hii tunajifunza somo la upendo ambao tunapaswa kujumuika pamoja katika sikuku hii ili tusherekee kufufuka kwa BWANA WETU YESU KRISTO. sikuku njemaaaaaa
Subscribe to:
Posts (Atom)