Umebaki mda mchache katika chuo kikuu cha dodoma kujiandaa na uchaguzi wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo. Mimi kama mdau wa globu ya mtandao vijana napenda kuwahimiza wanachuo wote kuwachagua viongozi ambao wanajali maslahi ya wanafunzi na sio uongozi wa chuo. Mwaka jana tulivutwa sana na siasa zinazongumzia sana umaskini na sio maslahi halisi, na tukavutwa kuwachagua viongozi ambao wametumia nafasi kuwa wao ni watoto wa mkulima na watajali maslahi kijana maskini. lakini tofauti na matarajia ya wengi hayo hayakutokea.
Mimi nawakumbusha tu kwamba siasa ni nzuri na maamuzi makubwa ni wanachuo wanahitaji kiongozi wanamna gani hasa kwa chuo hiki kichanga lakini kitakuwa kikubwa sana Afrika mashariki na kati. napenda kunukuu kutoka kwa rahisi wa marekani Abraham lincolin yeye alisema "politics is a nice game because it has no permanent friend and permanent enemy" siasa ni mchezo mzuri kwa sababu hauna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu. Kwa hiyo tusijenge uadui na viongozi wa mwaka jana maana hii ndo siasa. Mi nawahimiza wote tujitokeze kuchukua fomu na kugombea nafasi mbalimbali kuanzia nafasi ya juu mpaka chini na tushiriki kikamilifu katika upigaji wa kura.
No comments:
Post a Comment