John Mnyika ambaye ni mwanasiasa na mgombea kupitia CHADEMA, atangaza adhma yake ya mabadiliko na uwajibikaji pale alipotangaza rasmi kujitosa kugombea tena ubunge jimbo la ubungo mwaka huu wa 2010. Mnyika amesema kwa sasa hatazungumzia sana ahadi zake wala ilani ya chama kwa sababu kipindi cha kampeni bado.
Mwanasiasa huyu amejaribu kuelezea wajibu wa mbunge katika nyanja kuu nne ambazo ni kusikiliza na kuwakilisha wananchi pili, kusikiliza na kuwajibisha serikali na viongozi wake, tatu ni kushiriki katika kutunga sheria na nne ni alisema ni upatikanaji wa huduma. Mnyika alisisitiza kuwa wabunge wengi wanawaza kuwa jukumu lao kubwa ni kutoa bidhaa kwa wananchi ambapo huacha Taifa katika hali ya umaskini.
Mnyika amesisitiza kuwa kila mmoja mwenye umri unaostahili kupiga kura ambapo ni miaka 18 na zaidi anapaswa kujiandikisha katika daftari la kupiga kura na kutumia nafasi yake hii kama Mtanzania kikamilifu ili aweze kuleta mabadiliko ya kweli. Hata mimi namuunga mkono kwamba kila mwananchi anapaswa kutumia nafasi yake kikamilifu hasa kwa vijana ambao ni tegemeo na mhimili mkubwa Taifa hili la Tanzania
No comments:
Post a Comment