KARIBUNI SA

Monday, March 29, 2010

JE WAJUA SIRI YA MWANAFUNZI BORA KIDATO CHA NNE MWAKA 2010


Immaculata Mosha (16) ameibuka mwanafunzi bora kwa mwaka 2004 katika matokeo ya kidato cha nne. Baraza la mitihani NECTA lilimtangaza Immaculata kuwa kinara baada ya kuwashinda watahiniwa wenzake wapatao 315,151 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana.Mwanafunzi huyo kinara kutoka shule ya sekondari St Marian alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi 84 waliofanya mtihani huo mwaka 2009 shuleni hapo

Immaculata ni mtoto wa mwisho kati ya watoto wa prof. Resto Mosha ambaye pia muhadhiri katika chuo kikuu cha kilimo SUA, na mama Agatha Mosha mhasibu wa NSSF mkoani humo,


Akielezea historia yake ya mwenendo wa masomo yake darasani Mosha, alisema, nyota yake kishule ilinaza kung’ara tangu akiwa kidato cha kwanza shuleni hapo muhula wa pili aliposhika nafasi ya kwanza darasani.“Nilianza kidato cha kwanza na katika mitihani ya muhula wa kwanza nilikuwa mtu wa nne darasani, niliongeza bidii na mwisho wa mwaka nilikuwa wa kwanza hadi namaliza kidato cha nne darasani sikuwahi kuachia hiyo namba,” alisema Immaculata.Amesema, katika mitihani ya mchujo wa kidato cha pili yeye alishika nafasi ya 7 Kanda ya Mashariki jambo ambalo pia lilimsukuma kufanya vizuri zaidi.

Immaculata aliyezaliwa katika Hospitali ya taifa Muhumbili, Mei 6 mwaka 1993 alianza elimu yake ya awali (chekechea) katika shule ya St. Ann mjini Morogoro na baadae kuanzia hapo darasa la kwanza hadi la tatu alipohama.Darasa la nne alihamia katika shule ya Msingi Mukidoma iliyopo mkoani Arusha alipo malizia darasa la 7 mwaka 2005 na baadaye kalijiunga na sekondari ya St. Marian mjini Bagamoyo.Mosha anasema, anamuombva Mungu amsaidie katika masomo yake ili ndoto yake ya kuwa mhandisi wa mitambo(Mechanics Engineer) itimie.“Napenda sana hapo baadae niwe Injinia, hivyo nitaongeza bidii na kumuomba Mungu sana anitimizie hiyo ndoto yangu,” alisema Immaculata.

Akizungumzia maisha binafsi anasema miongoni mwa vitu ambavyo havipendi ni vile ambavyo watu wanaweza kumhukumu mtu kutokana na mwonekano wake wa nje.“Sipendi sana watu ambao wana 'judge the book by its cover' bila ya kujua undani halisi wa mtu mwenye kama anaendana kweli na muonekano huo.Akiwa ni msichana mwenye kupenda sana kula wali nyama kuliko vyakula vyoyote, pia hupendelea kuvaa suruali na ndiyo vazi ambalo hulipenda na kinywaji chake kikubwa ni soda iitwayo Fanta.

Pia anapenda kuwausia wanafunzi wenzake hasa wasichana kutojihusiha na vitendo visivyo faa katika kipindi cha shule kwani anaamini kuwa ndiyo msingi mbaya wa maendeleo yao shuleni.“Mimi naamini kila kitu kina wakati wake, ukifika nitafanya hivyo ila kwa sasa sijawahi kujiingiza katika vitendo vya anasa na nawahusia wanafunzi wenzangu kuwa waachane na vitendo hivyo,” aliongeza Mosha.

No comments:

Post a Comment