Katika kusherekea kutimiza miakA tisa tangu kuanzishwa kwake, TYVA iliwakutanisha wanachama na wapenzi wake katika uwanja wa chuo cha Usatawi wa Jamii Kijito nyama ambapo mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu ilifanyika dhidi ya timu ya IPP media .
Katika mchezo huo wa kukata na shoka ambao ulikuwa na mashiko ya aina yake, TYVA iliambulia kichapo cha mabao saba kwa moja shukrani kwa juhudi za Beno malisa aliyelisakama lango la IPP na kusababisha bao hilo.
Kwa ujumla meneja masoko wa IPP alikisifu kikosi cha TYVA ambacho kiliunda pia na maveterani kama Erick Ongara, Beno Malisa na Eliah Yobu. Alitanabaisha kuwa endapo timu ya TYVA ingekuwa imefanya mazoezi ya kutosha basi anaamini hadithi ingekuwa nyingine.
Katika tukio hilo lililochgizwa na uwepo wa wakongwe wengine kama Baruani mshare, mwenyekti wa kwanza wa asasi, Masozi Nyirenda, Elly Mgumba, Leah Ipini alikuwa akitimiza miaka 19 tangu kuzaliwa kwake hivyo kuamua kukata keki kwa niaba ya mtoto TYVA na ya kwake mwenyewe na kuwalisha wageni waliohudhuria mechi hiyo.
Wakitoa maoni yao kuhusiana na tukio hilo, Baruani Mashare na Erick Ongara walisema wamejisikia furaha ya aina yake kuunganika na kizazi kipya cha TYVA ambapo mwisho wa siku ni furahaa kwa wanaTYVA wote kama familia iliyo na malengo ya kuona ustawi wa jamii ambapo vijana ndio msingi wa maendeleo. Pia kubugizwa mabao mengi kiasi hicho hakikuwa kigezo cha kuvunja furaha ya siku kwani mechi yenyewe ililenga katika kuwaleta pamoja wanaTYVA na vile vile kujenga udugu na kampuni hiyo ya habari Tanzania.
Akitoa shukrani zake kwa mwaliko waTYVA wa kusherekea miaka hiyo tisa tangu kuanzishwa kwake, meneja masoko wa IPP media ailisema kuwa itakuwa vizuri kama TYVA ikiomba kucheza michezo mingine kama vile basketiball ili kuendelea kuupalilia udugu huo ulioanzishwa.
No comments:
Post a Comment