Jumapili ya tarehe 18/12/2010 usiku kumkia jumatatu wanachuo wa skuli ya sayansi ya jamii na sayansi ya lugha walianza mgomo wa kuishinikiza serikali juu ya matatizo yanayowakabili. Moja ya matatizo yaliyoanishwa na bunge la serikali ya wanafunzi ambalo lilibariki na kupitisha mgomo huu ni kutokuwepo kwa mafunzo ya vitendo kwa baadhi ya kozi zipatazo kumi na nne katika skuli hii.Madai ya wanafunzi hawa yamekuwa hayasikilizwi na kusababisha waamue kuandamana hadi kwa waziri mkuu mheshimiwa Mizengo Pinda.
Kulia mwenye koti la kijani ni Leonard Singo ambaye ni Rais wa skuli ya sayansi ya jamii na sanaa ya lugha (CSSH) akiongea na mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Msekela baada ya maandamano kuzuiwa na askari polisi kwenye lango la kuingia chuoni na katikati ni Mkuu wa skuli hii Pro. Casmir Rubagumya
Hapa ni mlezi au dean of student Mr.Manongi akiteta jambo
Askari wa kutuliza ghasia FFU wakiwa tayari kusubiri amri ya kutoa kichapo siku hiyo
wanachuo wakiwa tayari kwa lolote na wengi wao wakiwa wamebeba maji kwa ajili ya kunawa uso kupunguza adha ya mabomu ya machozi kama mmoja wapo anayeonekana kwenye picha hii.
hapa ndo maandamano yalipoanza kuvurigika na kila mtu kuchukua njia yake
No comments:
Post a Comment