KARIBUNI SA

Thursday, December 30, 2010

BOBBY FARREL WA BON M AFARIKI DUNIA


Boby Farrell wa BON M wakati wa uhai wake

Boby Farrell wa BON M afariki dunia mjini St.Petersburg,Urusi

Boby Farrell (61) alikuwa mwanamuziki mashuhuri katika miaka 1970 kutoka kundi maarufu enzi hizo linalofahamika kama Boney M,Mr. Boby Farrell amekutwa amefariki katika chumba cha hoteli alichofikia huko mjini St.Petersburg, Urusi.

Mwanamuziki huyo alikuwa katika ziara ya kimziki nchini Urusi, maiti yake iligunduliwa katika chumba alichofikia baada ya kumaliza show zake.idara ya usalama ya St.Peterburg imeunda kamati maalum ya kuchunguza kifo cha Bobby Farrell.

Marehemu Bobby Farrell alikuwa mwanamuziki anayeongoza safu ya mbele iliyokuwa bendi maarufu duniani Boney M, ambapo alifanya kazi na mwanamuziki Maisie Williams, Liz Mitchel na Marcia Barret.

Kundi la Bon M lilijizolea umarufu kila kona duniani kutokana na umahiri wa nyimbo zake kutingisha katika madisco na redio za kimataifa. Kundi hili lilikuwa na maskani yake nchini Ujerumani na kuweza kupiga tour kila kona duniani.

Baada ya kundi la Bon M kusambaratika marehemu Bobby Farrell alihamishia makazi yake mjini Amsterdam, Uholanzi.

Bobby Farrell ambaye ametamba na nyimbo zake akiwa na Boney M ambazo hupendwa sana kipindi hiki cha kusherekea Christmas na mwaka mpya hatunae tena duniani. Bobby Farrell ni moja ya wanamuziki watanashati sana duniani.

No comments:

Post a Comment