KARIBUNI SA

Monday, March 29, 2010

UDOM UCHAGUZI WA VIONGOZI UMEKARIBIA

Umebaki mda mchache katika chuo kikuu cha dodoma kujiandaa na uchaguzi wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo. Mimi kama mdau wa globu ya mtandao vijana napenda kuwahimiza wanachuo wote kuwachagua viongozi ambao wanajali maslahi ya wanafunzi na sio uongozi wa chuo. Mwaka jana tulivutwa sana na siasa zinazongumzia sana umaskini na sio maslahi halisi, na tukavutwa kuwachagua viongozi ambao wametumia nafasi kuwa wao ni watoto wa mkulima na watajali maslahi kijana maskini. lakini tofauti na matarajia ya wengi hayo hayakutokea.



Mimi nawakumbusha tu kwamba siasa ni nzuri na maamuzi makubwa ni wanachuo wanahitaji kiongozi wanamna gani hasa kwa chuo hiki kichanga lakini kitakuwa kikubwa sana Afrika mashariki na kati. napenda kunukuu kutoka kwa rahisi wa marekani Abraham lincolin yeye alisema "politics is a nice game because it has no permanent friend and permanent enemy" siasa ni mchezo mzuri kwa sababu hauna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu. Kwa hiyo tusijenge uadui na viongozi wa mwaka jana maana hii ndo siasa. Mi nawahimiza wote tujitokeze kuchukua fomu na kugombea nafasi mbalimbali kuanzia nafasi ya juu mpaka chini na tushiriki kikamilifu katika upigaji wa kura.

KUMBE NA OBAMA NAYEEE YUMOO.


Huyu mtoto wa ukweli anajisemeaaaa..........................!


jamani dada zetu hawa hata huku vyuoni saa nyingine hata masomo hayaendi , sasa inakuwaje kwa waheshimiwa kama huyu.? bodi gadi naye anamshangaa muheshimiwa. badala ya kumshtua anabaki kumtizama....!!!!!!

HUU NDIO MUONEKANO WA CHUO KIKUU DODOMA (UDOM)


Chuo kikuu dodoma ambacho kipo makao makuu ya Tanzania kitakuwa ni moja kati ya vyuo vikuu vikubwa Afrika mashariki na kati. Chuo hichi ambacho kinaendelea kujengwa na kinategemea kuchukua wanafunzi wapatao elfu arobaini kitakapomalizika katika stashahada na shahada tofauti

haya ni moja ya madarasa ambapo wanafunzi wa chuo kikuu dodoma wanayatumia kwa sasa, madarasa haya yanajulikana kama lecture room. pamoja na miundo mbinu mizuri ambayo serikali imeyatoa bado idadi ya waadhiri ni wachache hapa udom ambao husababisha waalimu ambao wanategemea kuwa wale ambao wanajulikana kamba flight lecture. Mimi kama mdau wa globu naipongeza serikali kwa miundo mbinu lakini naomba wawaatutafutie na waalimu maana ubora wa chuo si majengo bali ni elimu wanayoipata.

JE WAJUA SIRI YA MWANAFUNZI BORA KIDATO CHA NNE MWAKA 2010


Immaculata Mosha (16) ameibuka mwanafunzi bora kwa mwaka 2004 katika matokeo ya kidato cha nne. Baraza la mitihani NECTA lilimtangaza Immaculata kuwa kinara baada ya kuwashinda watahiniwa wenzake wapatao 315,151 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana.Mwanafunzi huyo kinara kutoka shule ya sekondari St Marian alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi 84 waliofanya mtihani huo mwaka 2009 shuleni hapo

Immaculata ni mtoto wa mwisho kati ya watoto wa prof. Resto Mosha ambaye pia muhadhiri katika chuo kikuu cha kilimo SUA, na mama Agatha Mosha mhasibu wa NSSF mkoani humo,


Akielezea historia yake ya mwenendo wa masomo yake darasani Mosha, alisema, nyota yake kishule ilinaza kung’ara tangu akiwa kidato cha kwanza shuleni hapo muhula wa pili aliposhika nafasi ya kwanza darasani.“Nilianza kidato cha kwanza na katika mitihani ya muhula wa kwanza nilikuwa mtu wa nne darasani, niliongeza bidii na mwisho wa mwaka nilikuwa wa kwanza hadi namaliza kidato cha nne darasani sikuwahi kuachia hiyo namba,” alisema Immaculata.Amesema, katika mitihani ya mchujo wa kidato cha pili yeye alishika nafasi ya 7 Kanda ya Mashariki jambo ambalo pia lilimsukuma kufanya vizuri zaidi.

Immaculata aliyezaliwa katika Hospitali ya taifa Muhumbili, Mei 6 mwaka 1993 alianza elimu yake ya awali (chekechea) katika shule ya St. Ann mjini Morogoro na baadae kuanzia hapo darasa la kwanza hadi la tatu alipohama.Darasa la nne alihamia katika shule ya Msingi Mukidoma iliyopo mkoani Arusha alipo malizia darasa la 7 mwaka 2005 na baadaye kalijiunga na sekondari ya St. Marian mjini Bagamoyo.Mosha anasema, anamuombva Mungu amsaidie katika masomo yake ili ndoto yake ya kuwa mhandisi wa mitambo(Mechanics Engineer) itimie.“Napenda sana hapo baadae niwe Injinia, hivyo nitaongeza bidii na kumuomba Mungu sana anitimizie hiyo ndoto yangu,” alisema Immaculata.

Akizungumzia maisha binafsi anasema miongoni mwa vitu ambavyo havipendi ni vile ambavyo watu wanaweza kumhukumu mtu kutokana na mwonekano wake wa nje.“Sipendi sana watu ambao wana 'judge the book by its cover' bila ya kujua undani halisi wa mtu mwenye kama anaendana kweli na muonekano huo.Akiwa ni msichana mwenye kupenda sana kula wali nyama kuliko vyakula vyoyote, pia hupendelea kuvaa suruali na ndiyo vazi ambalo hulipenda na kinywaji chake kikubwa ni soda iitwayo Fanta.

Pia anapenda kuwausia wanafunzi wenzake hasa wasichana kutojihusiha na vitendo visivyo faa katika kipindi cha shule kwani anaamini kuwa ndiyo msingi mbaya wa maendeleo yao shuleni.“Mimi naamini kila kitu kina wakati wake, ukifika nitafanya hivyo ila kwa sasa sijawahi kujiingiza katika vitendo vya anasa na nawahusia wanafunzi wenzangu kuwa waachane na vitendo hivyo,” aliongeza Mosha.

Sunday, March 28, 2010

KASHFA ZA NGONO ZALIKUMBA KANISA KATOLIKI


Kwa muda mrefu sasa Kanisa Katoliki limejikuta likigubikwa na kashfa za ngono.Hivi karibuni pepo mbaya amezidi kulizungukia Kanisa hio baada ya taarifa kwamba kaka wa Baba Mtakatifu,Georg Ratziger, aliwatangwa makofi wanakwaya wake katika miaka ya 1960.Kwa kitambo sasa,inaonekana Kanisa limekumbwa na jukumu kubwa la kuomba msamaha kutokana na tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia (na ulawiti) sambamba na jitihada za kusafisha sura yake.Hata hivyo,pamoja na kuendelea kuibuka kwa tuhuma hizo zisizopendeza,Kanisa Katoliki limeendelea kubaki 'safi' barani Afrika.Je hali hiyo inasababishwa na nini?Na je itaendelea kwa muda gani?Binafsi siamini kwamba tuhuma zinazolikabili Kanisa hilo haziligusi Bara la Afrika,na hususan Tanzania.Tofauti iliyopo ni kwamba imani za kiroho katika nchi zilizoendelea zina tofauti ya namna flani na ilivyo katika nchi zinazoendelea.Yayumkinika kusema watumishi wa Bwana katika nchi kama Tanzania wameendelea kunufaika na unyenyekevu uliokubuhu kutoka kwa waumini wao ilhali katika nchi za Magaharibi imani haimaanishikufumbia macho mauvu ya wasimamizi wa imani hiyo (i.e. watumishi wa Bwana).

Nadhani si mie peke yangu ninayefahamu kwamba baadhi ya watumishi wa Bwana wana watoto,kinyume kabisa na kanuni na taratibu za Kanisa Katoliki.Katika jimbo nililozaliwa,suala hilolinaonekana la kawaida sana kiasi kwamba baadhi ya watumishi wa Bwana wanamudu kuhudumia 'familia' zao (wanawake waliowapa ujauzito na kupata watoto wa wachunga kondoo wa Bwana) pasipo kificho.

Utumishi wa Bwana katika nchi yetu hauna tofauti sana na kinachoendelea kwenye siasa zetu.Tunafahamu wanasiasa wabovu lakini kwa vile wanamwaga vijizawadi hivi na vile tunaendelea kuwalea na hatimaye wanaoendelea kuipeleka mrama nchi yetu.Waumini wengi wa Kanisa Katoliki huko nyumbani wanafahamu fika maovu yanayotendwa na BAADHI ya watumishi wa Bwana lakini wanaendelea kufumbia macho.Natambua kuwa Maandiko Matakatifu yanasisitiza kuzingatia zaidi maneno/mafundisho ya viongozi wetu wa dini na sio kutilia mkazo mateno yao,lakini ni dhahiri padre mzinzi hawezi kuwa na mamlaka ya kiroho (moral authority) kukemea uvunjaji wa amri ya sita.

Na kuna imani kwamba kusuasua kwa baadhi ya viongozi wa dini huko nyumbani kukemea ufisadi na maovu mengine ya wanasiasa kunasababishwa na ukweli kwamba baadhi ya viongozi hao wa dini wanatambua kuwa 'hawako safi kihivyo'.Kama ilivyokuwa wakati wa sakata kati ya serikali na madhehebu ya dini kuhusu ushuru katika bidhaa zinazoingizwa nchi na madhehebu hayo,ambapo baadhi ya wanasiasa walidiriki kusema 'wanafahamu mengi kuhusu baadhi ya viongozi hao wa dini' ni dhahiri wachunga kondoo wa Bwana wanafahamu fika kuwa matendo yanayokiuka maadili yao yanafahamika na wanasiasa wangeweza 'kuwaumbua' kwa kuyaweka hadharani.

Hakuna anayefahamu hatma ya pepo huyu mchafu anayelitesa Kanisa letu lakini kilicho bayana ni athari zake kwa kondoo wa Bwana.Tayari kuna taarifa kwamba kuna mtikisiko wa kiimani katika nchi zinazofahamika kama vinara wa Ukatoliki kwa mfano Ujerumani,Austria na Ufaransa.Hali pia si shwari huko Vatican kiasi kwamba 'mpunga mapepo mkuu' (chief exorcist) katika makao makuu ya Kanisa hilo,Father Gabriel Amorth alinukuliwa akisema kuwa shetani ameweka makazi yake sehemu hiyo.

Wakati Kanisa Katoliki barani Afrika,Tanzania included,likiwa shwari katika kipindi hiki cha upepo mbaya wa shetani,ni muhimu kwa wachunga kondoo wa Bwana wanaokiuka mafundisho ya Kanisa hilo kujirudi wakitambua kuwa siri zao haitadumu milele.Pia ni muhimu kwao kufahamu kuwa japo wanasitiriwa kutokana na unyenyekevu uliopitiliza wa waumini wao,Mungu wanayemtumikia anaowaona na anakasirishwa sana.Japo wanaweza kuendelea kusalimika kutokana na waumini kuendelea 'kuwafumbia macho',ni dhahiri kuwa wasipobadilika wataishia kuwa kuni za kuchochea moto unaowachoma wadhambi huko 'motoni'.

Juma Kuu linapaswa kuwa kipindi kizuri kwa Kanisa Katoliki kila mahali kungalia wapi limejikwaa (na sio lilipoangukia) na kisha kufanya marekebisho yanayostahili.Na kwa Nguvu za Bwana,yote yanawezekana.

JAKAYA ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI


Rais Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, kutokana na vifo vya watu 10 waliopoteza maisha kwa ajali ya barabarani.

Ajali hiyo ilitokea juzi eneo la Kibamba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam baada ya lori kubwa la mafuta lenye tela, kugongana na basi dogo la abiria aina ya Hiace na hatimaye kulilalia na kusababisha watu wote waliokuwemo kwenye basi hilo kufariki dunia.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, jijini Dar es Salaam jana ilisema kupitia kwa Lukuvi, Rais Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa wote walipoteza ndugu zao katika ajali hiyo mbaya.

“Kupitia kwako, ninatuma salamu za rambirambi kwa watu wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika ajali hiyo mbaya,” alisema.

Aliongeza: “Ninaelewa fika ni kwa kiasi gani hivi sasa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wanaelemewa na huzuni kubwa na majonzi baada ya kuwapoteza wapendwa wao.”

Taarifa ilisema Rais Kikwete amewaomba wafiwa wote wawe na moyo wa uvumilivu na ujasiri wakati huu mgumu wa maombolezo ya vifo vya ndugu, jamaa na marafiki zao na amemuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi.

Katika salamu zake hizo, Rais Kikwete, amezisisitizia mamlaka zinazohusika na Sheria ya Usalama Barabarani, kuisimamia kikamilifu sheria hiyo ili Taifa lisiendelee kupoteza watu wake kutokana na kukiukwa kwa sheria hiyo.

MBOWE AHUTUBIA DODOMA


Mwenyekiti wa Chadema cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akihutumbia mkutano wa hadhara ikiwa ni mfululizo wa mikutano ya operesheni Sangara katika kata ya Ipera jimbo la Kibakwe mkoani Dodoma.

Tuesday, March 23, 2010

WANACHUO IFM WAGOMA


Madenti wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) jana waligoma kuingia darasani. Mgomo uliosababisha na kile ambacho madenti hao walichokilalamikia kupanda kwa ada pasipo mpangilio na taarifa yoyote. madenti hao ambao wengi wao wanasoma katika chuo hicho kwa ufadhili wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB) wanalalamika kuwa bodi haiwezi kuongeza ada kwa kiasi kilichoongezeka. madenti hao wamedai kuwa hawaitambui serikali ya wanafunzi katika chuo hicho kwa sababu haijatoa tamko lolote hadi wao walipofikia hatua ya kugoma. pia wanachodai mpaka sasa ni matokeo yao ambayo hawajayapata. Jamani sisi watoto wa maskini tuliopo vyuoni kwa nini tunanyanyaswa hivi, mhusika fikiri na kisha chukua hatua?

HIKI NI KIPIMO CHA AKILI


Tunaelekea uchaguzi mkuu mwaka huuuuu, je tupo tayari ?

MNYIKA ATANGAZA RASMI KUGOMBEA UBUNGE TENA


John Mnyika ambaye ni mwanasiasa na mgombea kupitia CHADEMA, atangaza adhma yake ya mabadiliko na uwajibikaji pale alipotangaza rasmi kujitosa kugombea tena ubunge jimbo la ubungo mwaka huu wa 2010. Mnyika amesema kwa sasa hatazungumzia sana ahadi zake wala ilani ya chama kwa sababu kipindi cha kampeni bado.

Mwanasiasa huyu amejaribu kuelezea wajibu wa mbunge katika nyanja kuu nne ambazo ni kusikiliza na kuwakilisha wananchi pili, kusikiliza na kuwajibisha serikali na viongozi wake, tatu ni kushiriki katika kutunga sheria na nne ni alisema ni upatikanaji wa huduma. Mnyika alisisitiza kuwa wabunge wengi wanawaza kuwa jukumu lao kubwa ni kutoa bidhaa kwa wananchi ambapo huacha Taifa katika hali ya umaskini.

Mnyika amesisitiza kuwa kila mmoja mwenye umri unaostahili kupiga kura ambapo ni miaka 18 na zaidi anapaswa kujiandikisha katika daftari la kupiga kura na kutumia nafasi yake hii kama Mtanzania kikamilifu ili aweze kuleta mabadiliko ya kweli. Hata mimi namuunga mkono kwamba kila mwananchi anapaswa kutumia nafasi yake kikamilifu hasa kwa vijana ambao ni tegemeo na mhimili mkubwa Taifa hili la Tanzania

Monday, March 22, 2010

HABARI MPYA KWA WANACHUO


international student week of Tanzania inayoandaliwa kwa ushirikiano wa chuo kikuu cha Dar es salaam inatoa nafasi kwa ajili ya kila mwanafunzi kuomba nafasi ya kushiriki katika matukio yatakayofanyika mapema mwaka huu. kwa taarifa zaidi tembelea web site yao www.iswt.or.tz. itumie nafasi hii kikamilifu

SIASA NA VITUKO VYA KAMANDA IDD AMINI DADA


His Excellency, President for Life, Field Marshal Al Hadji Doctor Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, Lord of All the Beasts of the Earth and Fishes of the Seas and Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular.
---------------------------------------------
Wapenzi wa dau wa globu ya mtandao wa vijana leo ninapenda kuwaletea moja ya hotuba ambayo ilitolewa na idd amin dada, mwanasiasa, mwanajeshi na aliyejipa kila aina ya vyeo vilivyokuwepo duniani.
HOTUBA ZA FILDI MASHO DOKTA AL HAJ IDI AMIN DADA
What you are about to read is REAL! Its not meant to serve as a ridicule. Below is an extract of one of dictator Iddi Amin's infamous speeches he used to deliver during the national celebrations. This particular speech was delivered in the U.K at the Conference of the U.N General Assembly.
------------------------
Ladies and women, my beloved husbands and men in this assembly, I am thank you very difficult for you hand to forgive me this hour to stalk of you Africa and my country which is Uganda. As I am a field marshall Dr. Or Haj Amin the Life President of my country, I am apologised because I have not deaded Archbishop Haemeni Kuvum. When many people tell me so many questions about him. His death on my behalf has happened with accident which was in the car when he yalked with it. So I am not a mistake you see.
Another words if or the order in my country in Uganda. The pressnewsmen which you can look them there will wanted to know the law orders of my country. They have inquiring me many questions in because my policemen don't catch people in court while they lost them on the way. No this is not right, yet all them who are catched by my policement are removed for court. When the court does not find them good enough and tie them all with mistakes begining from one month through to ten years with even above.
So we attempt people in the court before we tie them to prisons and those you understand about they dead are with if they travel dead themselves. Man invent their death. Uganda is peace loving brother country when people enjoy as if they are in another country. That is true about the country.
Dr. Kurt Waldeheim, you are beautiful in one of these husbands. I think you are this beauty to look what is going on in South Africa with Rhodesia, I am sending two hours to whites as if they can choose freedom to Africa, brothers or you will not blame me as I take wondering action to blow them. Israel is another enemy, they deaded sleeping soldiers of Uganda when they find them at night in Intebbe.
I walked one morning and I invented bodies of my soldiers sleeping in the airport and Israel had deaded people there. They must see or because I pay them of this bad news. Last of that I am thank your lunch which smelled good I am again fed up with it and have admitted revenge when both of you are invited by Uganda.
Thank you very hard and we shall collide everywhere in internal matter like assembly.
Thank you very hard. --
Field Marshall Dr. V.C. DSO M.C. Amin, Conquerer of the British Empire
------------------------
The pressmen, when asked by the Queen as to what President Amin has said, replied: "Your Majesty, That was President Amin of Uganda speaking a language similar to English."

Friday, March 19, 2010

ASASI YA DIRA YA VIJANA YAAZIMISHA TYVA DAY

Katika kusherekea kutimiza miakA tisa tangu kuanzishwa kwake, TYVA iliwakutanisha wanachama na wapenzi wake katika uwanja wa chuo cha Usatawi wa Jamii Kijito nyama ambapo mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu ilifanyika dhidi ya timu ya IPP media .

Katika mchezo huo wa kukata na shoka ambao ulikuwa na mashiko ya aina yake, TYVA iliambulia kichapo cha mabao saba kwa moja shukrani kwa juhudi za Beno malisa aliyelisakama lango la IPP na kusababisha bao hilo.

Kwa ujumla meneja masoko wa IPP alikisifu kikosi cha TYVA ambacho kiliunda pia na maveterani kama Erick Ongara, Beno Malisa na Eliah Yobu. Alitanabaisha kuwa endapo timu ya TYVA ingekuwa imefanya mazoezi ya kutosha basi anaamini hadithi ingekuwa nyingine.

Katika tukio hilo lililochgizwa na uwepo wa wakongwe wengine kama Baruani mshare, mwenyekti wa kwanza wa asasi, Masozi Nyirenda, Elly Mgumba, Leah Ipini alikuwa akitimiza miaka 19 tangu kuzaliwa kwake hivyo kuamua kukata keki kwa niaba ya mtoto TYVA na ya kwake mwenyewe na kuwalisha wageni waliohudhuria mechi hiyo.

Wakitoa maoni yao kuhusiana na tukio hilo, Baruani Mashare na Erick Ongara walisema wamejisikia furaha ya aina yake kuunganika na kizazi kipya cha TYVA ambapo mwisho wa siku ni furahaa kwa wanaTYVA wote kama familia iliyo na malengo ya kuona ustawi wa jamii ambapo vijana ndio msingi wa maendeleo. Pia kubugizwa mabao mengi kiasi hicho hakikuwa kigezo cha kuvunja furaha ya siku kwani mechi yenyewe ililenga katika kuwaleta pamoja wanaTYVA na vile vile kujenga udugu na kampuni hiyo ya habari Tanzania.

Akitoa shukrani zake kwa mwaliko waTYVA wa kusherekea miaka hiyo tisa tangu kuanzishwa kwake, meneja masoko wa IPP media ailisema kuwa itakuwa vizuri kama TYVA ikiomba kucheza michezo mingine kama vile basketiball ili kuendelea kuupalilia udugu huo ulioanzishwa.

UJASIRIAMALI KATIKA NIDO ZA JUISI


Katika ulimwengu huu wa sasa, watu wanajaribu kuwa wabunifu katika swala zima la ujasiriamali hasa kwa sababu ya ushindani wa kibiashara. huku kwetu ulaya wadada wameamua kubuni biashara ya nido za juisi ambapo mtu unanua nido moja ya juisi kwa thamani ya US dollar 10. picha hapo juu inaonyesha jinsi huduma hii inavyotolewa hasa mijini na kupata wateja wengi sana.

Tuesday, March 16, 2010

VIONGOZI WA LOYOLA ALUMNI ASSOCIATION( LAA) WATEMBELEA UDOM


Mwisho wa wiki tarehe 13 mwezi wa 3 mwaka huu 2010, viongozi kutoka makao makuu ya asasi ya wanafunzi waliosoma katika shule ya Loyola walitembelea chuo kikuu cha dodoma na kujiona mazingira mazuri ya chuo ambacho kinaendelea kujengwa. viongozi hao ambao ni janeth ambaye ni katibu, joseph ambaye ni muheka hazina, felix na sia lyimo wote ambao ulikuwa ni msafara wa watu wanne. siku hiyo viongozi hao walipata mda wa kuongea na wanafunzi ambao walimaliza shule ya loyola na sasa wanachukua shahada yao katika chuo hicho. walisisitiza sana juu ya kuwa na upendo na kauli mbiu yao inayosema "men and women for others". baada ya kutoa nasaha zao wanafunzi hao walipata mda wa kuimba wimbo wao wa taifa wakiwepo chuon hapo. viongozi hao waliwashukuru sana viongozi wa asasi katika chuo kikuu cha dodoma kwa mapokezi mazuri.