KARIBUNI SA

Monday, August 1, 2011

J sisters wazindua album ya CHUKUA USHINDI jana jumapili

Kundi la Muziki wa Injili la J SISTERS linaloundwa na wanamuziki ndugu JENNIFER(kulia pichani), JESSICAR (katikati) , JAQUILLINE (kushoto Pichani) na JULIET limezindua albamu yao ya tatu inayojulikana kama CHUKUA USHINDI jana Jumapili hii ndani ya ukumbi wa DIAMOND JUBILEE jijini Dar es salaam.Uzinduzi huu unafuatiwa baada ya kufanya uzinduzi mwingine wiki mbili zilizopita katika uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma.

Mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, pia uzinduzi huo ulisindikizwa na waimbaji wengine maarufu wa muziki wa Injili nchini kama Frola Mbasha, Bonny Mwaitege, Martha Maipaja na wengine wengi. Kiingilio cha juu kilikuwa ni shilingi 10,000, 5,000 na 3000 kwa watoto.

No comments:

Post a Comment