KARIBUNI SA

Wednesday, April 21, 2010

UCHAGUZI UDOSO WAZINDULIWA RASMI JUMATANO YA TAREHE 15.04.2010

siku ya jumatano iliyopita chuo kikuu cha Dodoma,uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ulizinduliwa rasmi na mlezi wa wanafunzi au dean of student katika ukumbi mkubwa chimwaga ukifuatiwa na mdahalo wa viongozi ambao wanagombea nafasi mbalimbali ikiwemo mwenyekiti wa chuo kizima na makamu wenyeviti wa kila kitivo, mlezi huyo wa wanafunzi alisisitiza kuwa tunabidi tufanye siasa kwa amani na tusichafue majina ya watu kama mwaka jana ilivyokuwa katika uchaguzi wa pili wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu hiki ambacho kinategewa kuwa chuo kikubwa afrika mashariki na kati. Mlezi huyo aliendelea kusisitiza kwamba wote tunapaswa kushiriki kwenye uchaguzi huu kwa njia ya amani na tuchague viongozi tunaowahitaji. Alitoa mfano wa chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda ambapo mwanzo mwa mwaka huu wanafunzi walipoteza maisha kutokana na shughuli za kisiasa ambazo zilikuwa zikiendelea hapa. Pia mlezi huyo aliendelea kusema kwamba wao kama utawala watakuwa bega kwa bega kusimamia uchaguzi huo ufanyike kwa njia ya amani


Hapa chuoni michakato ya kuunda kambi inaendelea ambayo inaonyesha kila mmoja yupo kimaslahi zaidi ya kupata uongozi na kuendeleza usela au ushikaji. Mwaka jana yalitokea kama haya ambapo muheshimiwa Teri Gilead ambaye alikuwa mpinzani mkubwa wa Ambrose alikuwa na haya ya kusema pale alipohojiwa na Kubwakuliko alikuwa na haya ya kusema

Mgombea Urais aliyepita ssh
Muheshimiwa Gilead Terry

TERRY: Kwanza napenda kukushukuru sana kwa kufika hapa, umekuwa kama tone la mvua jangwani. Serkali hii bana ni serikali ya kishkaji mnoooo
MWANDISHI: Una maanisha nini mkuu?
TERRY: Yaani, uwezi kuamini waziri mkuu wenu ni mwanachumba mwenzake “roommate” athari ya hili ndo kama unavyo ona sasa anakuwa anamjali yeye zaidi kulliko watu wengine
MWANDISHI: Alikuwa roommate wake kabla au baada ya kuwa Rais?
TERRY: Kabla ya kuwa rais, kifupi ni kwamba serikali haikujiaanda kabisa kuongoza ,wanavyo tufanyia ni, “foolishness of the highest level”
Sasa ni vyema kufanya maamuzi ambayo yatatuletea maslahi makubwa kwetu kwa kipindi kijacho na sio maslahi binafsi. Maana kuna msemo usemao “ SI KILA AKUTAZAMAYE ANAKUONA” kwa hiyo tusiwatupia mpira wengine kwamba wao ndo wahusika lakini wote tunapaswa kushiriki pamoja katika hili
Kutoka kwa mdau
Manase Kavishe

No comments:

Post a Comment