Thursday, March 10, 2011
SERIKALI KUUNDA TUME YA KUCHUNGUZA DAWA YA BABU WA LOLIONDO.
WAKATI idadi ya watu ikizidi kumiminika katika Kijiji cha Samunge, Tarafa Sale, Loliondo kupata kile kinachoaminika kuwa ni tiba dhidi ya magonjwa sugu, kutoka kwa mtoa huduma Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Ambilikile Mwasapila
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hadji Mponda leo, amesema imetuma wataalamu ambao watakwenda huko Loliondo na kuangalia kama mazingira ya eneo hilo ni hatarishi kwa wagonjwa na kumshauri Babu Mwasapile ili aweze kusajili dayo katika mamlaka inayohusika na madawa yaani TFDA Akizungumza na waandishi wa habari katika Wizara hiyo leo Dr. Mponda, amesema kama Babu Ambilikile Mwasapila kama anataka kuendelea kufanya kazi hiyo, anatakiwa kufuata taratibu kwa kusajiri dawa hiyo katika Mamlaka ya Dawa na Vyakula TFDA ili iweze kuthibitishwakwa kama haina madhara yoyote
Kwa amri hiyo ya serikali inamaanisha kwamba, watu ambao wako huko Loliondo kwa minajili ya kupata matibabu, watalazimika kuondoka huko kwa kuwa hawataweza kupata matibabu.
Subscribe to:
Posts (Atom)