KARIBUNI SA

Friday, August 6, 2010

JK ALIPOMTEMBELEA OBAMA WHITE HOUSE

JK akibadilishana mawazo na Rais wa marekani Barrack Obama ndani ya ikulu ya marekani.Waafrika wengi walikuwa na moyo uliojaa matumaini pale walipoona Rais Obama ambaye ni mmarekani mwenye asili ya Afrika huko Kenya ambako ni Afrika Mashariki. Ndoto hizi ambazo zimetimia kwa sasa zilitabiriwa na mpigania haki za mtu mweusi huko Marekani aliyeitwa Dk.Martin luther King jr. siku moja wakati akiwahutubia Wamarekani alisema" nina ndoto kuwa siku moja watoto wangu watatu watatambulika, sio kwa sababu ya rangi ya ngozi zao bali ni uwezo walio nao"

Haya yanatimia baada ya kumuona Rais Obama akiliongoza taifa lenye uwezo na nguvu za kivita kama Marekani. Sasa je, hapa Rais JK alipopata nafasi ya kukutana na Obama unafikiri watazungumza nini kwa mara ya kwanza?

DK. SLAA AENDELEA KUNGURUMA NCHINI KUTAFUTA WADHAMINI


Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa akihutubia umati wa wakazi wa Mtwara alikoenda kutafuta udhamini

sehemu ya umati mkubwa wa wakazi wa Mtwara mkutanoni hapo


Mh. Mabere Marando akiongea wakati wa mkutano huo