KARIBUNI SA

Thursday, September 30, 2010

JK APIGA KAMPENI KUFA NA KUPONA

Wakati wengine wakilalamika kwamba hawaoni kilichofanyika bado wapo ambao wanatambua nafasi ya Rais ambaye amemaliza muda wake wa miaka 5. Muheshimiwa Jakaya Kikwete. Hii ni kutokana na kugusa maisha yao mojamoja kama ilivyotokea kwa Dada yetu Bahati ambaye ni mlemavu.

JK akiongea na Bahati Iddi Nzimano, mwanadada mwenye ulemavu wa kutokuwa na mikono yote miwili ambaye mwaka juzi alimsaidia mtaji wa kufungua biashara na sasa Bahati maisha yake ni mswano kabisa licha ya ulemavu alionao.
JE, HUU NI USHABIKI WA KISIASA AU NI UHALISIA WA MAMBO, WE WASEMAJE???

RAIS MSTAAFU BEN MKAPA ALAMBA DUME KWA BAN KI-MOON


Mh. Mkapa aliteuliwa wiki iliyopita na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Bw. Ban Ki-moon kuongoza timu ya watu watatu watakaofualitia na kuangalia kura ya maoni ya Sudan Kusini. Mh. Mkapa amesema kura hiyo ni ya muhimu sana kwa hatma ya mamilioni ya Wasudan ambao Januari tisa watapiga kura kuamua endapo eneo la Sudan Kusini lijitenge na kuwa taifa huru ama la na amesema la msingi ni kwa watu kukubali matokeo mara kura hiyo itakapokamilika.. Mh. Mkapa aliyazungumza hayo wakati wa mahojiano na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya Umoja wa Mataifa,B. Flora Nducha

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh. Benjamin W. Mkapa akiwa katika mahojiano na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa,Bi Flora Nducha katika ofisi za Umoja wa Mataifa,jijini New York,Marekani.


Kwa kusikiliza mahojiano hayo ingia katika mtandao wa Redio ya Umoja wa Mtaifa http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili pia kwenye facebook http://www.facebook.com/UNRadioKis au waweza kubonyeza moja kwa moja kwenye mahojiano yenyewe http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/detail/113198.html